William Tuva kuwalisha wazee 2000 wasiojiweza Kenya

[ad_1]

Kwa mafanikio aliyonayo mtangazaji wa kituo cha redio cha Citizen radio nchini Kenya almaarufu kama Mzazi Willy M Tuva, aliona ni vyema kukumbuka jamii kwa kuanzisha wakfu kwa jina Mzazi Foundation. Hakuna anayepinga kwa juhudi anazopiga katika kipaji chake cha utangazaji, na mamia ya vijana katika burudani la muziki ama ulingo wa sanaa kwa ujumla wamekua wakipata support ya nguvu kupitia mikono yake kote Afrika Mashariki.

Huenda moyo huu alionao kwa burudani la muziki, umempa msukumo wa kufanya makubwa zaidi katika jamii. Na moja wapo ya kuonyesha anashukuru jamii kwa kumpa fursa iliyomfikisha pale alipofika kimaisha, ameona hana budi kuwasaidia wanaohitaji katika jamii.

Umaarufu alionao, na jinsi anavyopendwa na mashabiki haswa vijana, unaongezea hatma yake hadhi na kibali kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuungana naye katika kuhakikisha ndoto yake yakusaidia jamii inatimia.
Jumapili 12/2/2017, akishirikiana na shirika la Old Is Diamond (OID) Tuva atakuwa katika maeneo ya Sagana kugawa chakula cha msaada kwa wazee wa eneo hilo na maeneo mengine nchini Kenya. Akitoa taarifa hiyo kupitia account yake ya Facebook, Tuva aliandika nikinukuu…

#MzaziFoundationCharityDrive #PassAHeart ; Old Is Diamond in conjuction with Mzazi Foundation hope to give foodstuffs to 500 elderly men and women from 5 very needy villages in Kamuthanga Mjini, Kijiji, Ngoka and Karima.
We will also be feeding 1,500 elderly people on a balanced diet on the d-day at upper Sagana primary school in Sagana. Following the drought situation in Kenya we humbly appeal for food donations to the grannies in the 5 mentioned villages. You can donate foodstuff that include cereals (maize, beans) maize flour, rice, cooking oil, potatoes, wheat flour. GOD BLESS YOU

Tuva anaingia kwenye list ya watu maarufu wanao rudisha kwa jamii, akiwemo msanii Jaguar kutoka Kenya, Eddy Kenzo kutoka Uganda, Diamond na wengine ambao kwa mara nyingi wamekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kile wanachokipata kwa kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Instagram: changez_ndzai
Twitter : ChangezN

[ad_2]

Source link

Leave a comment