Walter Chilambo – “sijawahi tumia milioni 50 za BSS kwenye muziki”

Mshindi wa shindano la Bongo Star Search 2013, Walter Chilambo amesema hajawahi kutumia pesa aliyoshinda kwenye Shindano hilo kwa shughuli zake za muziki.

maxresdefault (2)

“Milioni 50 nilizozipata nimezitumia kwa mambo mengine kabisa kama kununua gari na mengine ya kimaisha zaidi ya muziki, Chilambo aliiambia tovuti ya Times FM.

Chilambo amesema kazi zake za muziki zilikuwa zikisimamiwa na kampuni ya simu ya Zantel na wadau wengine wa muziki. “Kuna kipindi naenda studio, unakuta producer ananizawadia beat, nami kwakuwa ninaifanyia kazi nzuri basi sikatwi hela yoyote,” alisema.

Leave a comment