Sikutoa nyimbo sababu ya uchaguzi – Mwana FA

Baada ya kimya kirefu msanii Mwana F.A anatarajia kuachia baadhi ya kazi alizozifanya, na kuelekea nchini Afrika Kusini kufanya video zake na kuongeza orodha ya wasanii wanaotoka nchini na kwenda kufanya Video Afrika Kusini

Mwana F. A ameiambia Planet Bongo ya East africa Radio kuwa mishe za uchaguzi ndio zilimfanya asitoe nyimbo hizo.

“Kweli nina kazi wala sio kazi moja wala sio kazi mbili, yani nina kazi kadhaa na wiki ijayo narekodi nyingine, lakini haya mambo ya uchaguzi kila kitu kilikuwa Magufuli, Lowasa, kwa hiyo ikawa ngumu kidogo kutoa ngoma, watu hype ya uchaguzi ilikuwa kubwa sana, lakini now kwamba uchaguzi umekwisha tunataka kutoa ngoma na wikiendi hii naenda kufanya video South Africa”, alisema Mwana F.A.

Mwana FA aliendelea kwa kuthibitisha kuwa kipindi cha uhaguzi nyimbo nyingi ambazo zilitoka hazikufanikiwa kufanya vizuri.

“Ushahidi wa hilo unaweza kuona nyimbo nyingi ambazo zimetoka katika hiki kipindi cha karibuni zimeshindwa kufanya vizuri kwa sababu watu akili zao zote ziko kwenye siasa”, alisema F.A

Leave a comment