Ommy Dimpoz : Napenda kurusha fedha na mikufu kwa mashabiki jukwaani

Kila msanii hua na mzuka wake awapo jukwaani, hasa mashabiki wakiwa nyomi na shangwe zikitawala. Kwa upande Omary “Ommy Dimpoz” Nyembo mzuka wake huwa ni kuwarushia zawadi mashabiki wake.

Ommy2

Muimbaji huyo wa ‘Wanjera’ amesema kuwa hupenda kuwarushia vitu vyake mashabiki awapo jukwaani, kama ishara ya upendo wake kwao kutokana na kusupport kazi zake.

“Hakuna kitu ninachokipenda kama kurusha vitu vyangu mashabiki wangu nikiwa jukwaani hii inaonyesha jinsi gani nawapenda, lakini pia inaongeza burudani kwao huku wakiendelea kupenda shoo yangu na muziki wangu kwa ujumla,’’ Dimpoz aliliambia gazeti la Mtanzania.

Aliongeza kwamba kufanya hivyo kunamuongezea mashabiki na ufuatiliaji wa muziki anaofanya na wengi wao humfuatilia ili kujua maisha yake kwa ujumla.

 

Leave a comment