Muziki umenifanya nikosane na maboyfriend zangu – Queen Darleen

Queen Darleen ambaye pia ni dada yake na Diaqueen darleen bongobeatzmond amesema ameachana na wanaume wengi kutokana familia za wanaume kutomkubali kwa kudai ni mhuni.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio leo, Darleen alisema ndugu wa upande wa wanaume wamekuwa wakichochotea maneno kwa watoto wao hali iliyosabisha kuachana.
“Wachumba wachumba hawa, wanaume wanakuelewa lakini tatizo upande wa familia wanakuona mwanamke mhuni umeshindikana, umemaliza wasanii wote, kwamba huyo demu mhuni,” amesema. “Wanakuwa wanasema, nani huyo, huyo Queen Darleen, ndio mpenzi wako, ameshindikana na wanaume wote mjini, wasanii wote amewamaliza. Lakini sasa hivi kidogo napata afueni kwamba wazazi kidogo wamekuwa wanaelewa na wanapenda Bongo Flava, sema ndoa ndio inakuwa ngumu,” aliongeza.

Leave a comment